H HHA AAR RRRRI IISSSO OON NN UUU GGGIIRRL …harrisongirls.ac.tz/school_info/Form One (I)...
Transcript of H HHA AAR RRRRI IISSSO OON NN UUU GGGIIRRL …harrisongirls.ac.tz/school_info/Form One (I)...
Ukurasa wa 1 kati ya 15
HHHAAARRRRRRIIISSSOOONNN UUUWWWAAATTTAAA GGGIIIRRRLLLSSS’’’ SSSEEECCCOOONNNDDDAAARRRYYY SSSCCCHHHOOOOOOLLL
Email: [email protected]
Website: www.uwata.or.tz /
www.harrisongirls.ac.tz
“EDUCATION IS A SUSTAINABLE ASSET”
______________________________________________________________________________
YAH: TAARIFA YA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA
MWAKA 2020
Mzazi/Mlezi wa _________________________________
Ninafurahi kukutaarifu kuwa mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika
shule yetu. Hongera sana.
Shule inamilikiwa na Uamsho wa Wakristo Tanzania (UWATA) na inawapokea wanafunzi
kutoka mazingira mbalimbali pamoja na dini zote. Tunawalea wanafunzi kwa misingi ya
kumhofu na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, tunasisitiza nidhamu pamoja na kutoa Elimu
bora itakayomwezesha mwanafunzi kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha katika
ulimwengu wa Sayansi na Teknolojia.Hivyo uchaguzi wako wa kumleta mwanao Harrison
Uwata ni sahihi.
KARIBU SANA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA HARRISON UWATA
“Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee”
(Mithali 22:5)
Shule ni ya BWENI, hivyo utalazimika kugharimia gharama zote za mwanafunzi wa Bweni
kwa kufuata mchanganuo uliofafanuliwa katika fomu ya kujiunga na shule iliyoambatanishwa
na barua hii. Hata hivyo utatakiwa kujaza fomu zifuatazo na kuzirudisha siku ya kuwasili
shuleni.
1. Fomu ya uchunguzi wa Afya (Medical Examination Form)
2. Fomu ya taarifa binafsi za mwanafunzi.
3. Tamko rasmi la kukubali kujiunga na shule
4. Fomu ya utii wa sheria, kanuni za shule na Tabia njema.
Shule ipo jijini Mbeya eneo la Iwambi Mita50 kutoka barabara kuu iendayo Zambia upande
wa kusini mwa barabara.
● Wanafunzi wanaotokea mikoa ya kanda ya ziwa, kanda ya kati kanda ya
kaskazini,kanda ya magharibi, kanda ya mashariki na mikoa ya Iringa,Njombe na
Ruvuma wakifika stendi ya Nane nane au stendi kuu ya Mbeya wapande daladala
zinazokwenda Mbalizi na washuke kituo cha Iwambi.
Lakini pia wanafunzi wanaotokea mkoa wa Dar es salaam waweza kupanda mabasi
Ukurasa wa 2 kati ya 15
yaendayo Tunduma kisha washuke stand ya Iwambi.
● Wanafunzi wanaotokea Rukwa,Tunduma na Mbozi washuke kituo cha Iwambi
● Mwanafunzi akifika kituo cha Iwambi aweza kutembea kwa miguu kuelekea
mwelekeo wa bara bara iendayo Tunduma ambako baada ya mita chache mbele
ataona kibao cha HARRISON-UWATA upande wa kushoto kitakachomwelekeza
sehemu shule ilipo.
MUHIMU:
Mwanafunzi anatakiwa kuripoti shuleni siku ya Ijumaa tarehe 03/01/2020 bila kukosa.
Endapo atachelewa kuripoti kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe ya kufungua shule, nafasi
yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine.
SEHEMU A: MASOMO YANAYOFUNDISHWA KIDATO CHA KWANZA
Civics, History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic
Mathematics, Chemistry, Physics, Biology, Computer & Bible knowledge.
SEHEMU B:
1. GHARAMA YA ADA KWA MWAKA 2020.
Karo pamoja na gharama za Hosteli ni Tsh 2,100,000/=
S/N KIASI MUDA WA KULIPA
1 300,000/= Lipa kabla ya 02 Novemba, 2019 kwa ajili ya kushika nafasi.
Kushindwa kufanya hivyo nafasi yako atapewa mtu mwingine.
2 450,000/= Lipa kabla ya 02 Januari 2020
3 400,000/= Lipa kabla ya 03 Aprili 2020
4 550,000/= Lipa kabla ya 02 Julai 2020 5 400,000/= Lipa kabla ya 03 Septemba 2020
JUMLA 2,100,000/= Ilipwe kupitia akaunti ya shule
2. GHARAMA ZA MAHITAJI MENGINE
Na. MAHITAJI KIWANGO MAELEZO
1 Sare za shule 200,000/= Atapewa,sketi mbili, shamba dress moja, shati mbili,
t-shirt moja, tai mbili, sweta moja, jezi na suruali
yake, sketi ya michezo, trucksuit, mzura na gloves (za
kuvaa wakati wa baridi).
2 Mazingira, afya
na uchakavu
130,000/=. Uboreshaji mazingira, uchakavu wa samani za shule
na huduma ya kwanza
JUMLA 330,000/= Ilipwe kupitia akaunti ya shule
Akaunti za shule :
i. CRDB a/c no; 01j1065414702 (UWATA EDUCATION CENTRE)
ii. NMB a/c no; 62206600077 (HARRISON UWATA GIRLS’ HIGH SCHOOL)
Ukurasa wa 3 kati ya 15
MICHANGO YA KITAALUMA NA MAHITAJI YA MWANAFUNZI MWAKA 2020
A: MICHANGO YA KITAALUMA
Na AINA YA MCHANGO KIASI
1 Mtihani wa pamoja wa Jiji, Ujirani mwema pamoja na
masomo ya ziada (Remedial)
Tsh. 50,000/=
2 Rimu mbili za A4 (Rimu moja kwa kila muhula).
B: MAHITAJI YA MWANAFUNZI
Na AINA YA MCHANGO KIASI
1 Kulipia godoro kwa mwaka mzima.
Tsh. 20,000/=
2 Vyombo vya chakula (Sahani na kikombe) Tsh. 5,000/=
3 Fedha ya matumizi binafsi ya mwanafunzi (Pocket Money)
pamoja na kunyoa nywele.
Tsh. 107,000/=
(Tsh. 53,500/= kwa muhula).
NB:
Fedha hizi zote ziletwe mkononi siku ya kuripoti shuleni.
Ukurasa wa 4 kati ya 15
Tafadhali zingatia haya:
o Kulipa ada na michango mingine kwa wakati uliopangwa
o Ifahamike kwamba taasisi ya UWATA ina akaunti nyingi, hivyo zingatia kulipia kwenye
akaunti husika hapo juu.
o Kumbuka kuandika jina la mwanafunzi kwenye Bank pay in slip (risiti ya benki)
unapolipa ada na michango kwenye akaunti na uje nayo shuleni siku ya kuripoti.
Mahitaji mengine ya mwanafunzi anayotakiwa kuja nayo au kununua kwenye duka la shule ni
kama ifuatavyo:
(i) Blanketi moja. 1pc, @ 15,000/= au Tsh 35,000/=
(ii) Taulo mbili. 1pc @ 8,000/=
(iii) Khanga doti 2 @ Tsh 8,000/= au kitenge doti 2 @ 17,000/=
(iv) Shuka 2 (Moja rangi ya pinki na moja ya bluu) @ 6,500/=
(v) Ndoo moja ya kuogea na kufulia 3,500/=
(vi) Kijiko Tsh. 500/=
(vii) Toilet papers za kutosha @ Tsh. 1,000/=
(viii) Chandarua Tsh. 8,500/=
(ix) Aje na Raba nyeusi za michezo.
(x) Aje na Picha ndogo 4 (Passport size)
(xi) Pia anatakiwa kuja na nguo binafsi (za nyumbani) zisizozidi jozi mbili na ya tatu
atakayokuwa amevaa siku anapowasili shuleni, ziwe ndefu na zisizoangaza. Nguo /
Blauzi iwe na mikono mirefu au ikiwa ni mikono mifupi iwe usawa wa kiwiko cha
mkono.
(xii) Viatu vyeusi vyenye kisigino kifupi na vyenye kamba, jozi 2 (visivyo na kamba
haviruhusiwi) pamoja na viatu vyeusi vya wazi vyenye mkanda nyuma vya kushindia
(Flat Open shoes) jozi moja tu na ndala za kuogea na sio yeboyebo. Simple shoes
haziruhusiwi. (xiii) Soksi nyeupe za kutosha zenye urefu wa kati. @ 1,000/= (Soksi za rangi nyingine
iwayo yoyote haziruhusiwi).
(xiv) Jaketi la aina yoyote hairuhusiwi, isipokuwa sweta la shule tu.
(xv) Daftari kumi na moja (11) za aina ya kaunta (4 QUIRE) @ 4,500/= pamoja na daftari
ndogo kumi na moja za mazoezi zenye kurasa 200. @ 1,500/=
(xvi) Begi la saizi ya kati la kuhifadhia vitu vyake na sio sanduku la bati(Trunker)
(xvii) Vibanio vya kuanikia nguo(jozi mbili) @ 2,000/=
(xviii) Aje na brash ngumu ya mkono ya kusugulia sinki na squeezer (skwiza) yakusugulia
sakafu.
(xix) Aje na File kubwa la kuwekea mitihani yake (Box file) tsh. 3,500/=, kalamu za wino
(pens) zisizopungua kumi @ Tsh. 200/=, kalamu tatu za risasi (penseli), @ tsh. 100 au
tsh. 300. rula tsh. 500/= na mkebe tsh. 2,500/=
Mahitaji hayo yote pia yanapatikana kwenye duka la shule kwa gharama zilizoainishwa
hapo juu isipokuwa Viatu na Mabegi.
NB: Waweza kuwasiliana na wauzaji katika duka la shule kwa namba za simu 0755717362 au
0755486525.
Ukurasa wa 5 kati ya 15
MUHIMU:
Mzazi / Mlezi unatakiwa kumnunulia mwanafunzi vitabu vifuatavyo. Pia vinapatikana
kwenye duka la shule kwa bei zifuatazo:
i. Basic mathematics book one by TIE au by Oxford. Tsh. 15,000/=
ii. Biology Book1 & 2 by Oxford. Tsh. 15,000/=
iii. Chemistry Book 1 & 2 by TIE. Tsh. 18,000/=
iv. Physics Book 1 & 2 by TIE. Tsh. 18,000/=
v. Geography Book 1 & 2 by TIE. Tsh. 18,000/=
vi. History Book One by TIE. Tsh. 15,000/=
vii. Civics Book 1 & 2 by TIE. Tsh. 18,000/=
viii. Kiswahili Kidato cha Kwanza by Oxford. Tsh. 12,000/=
ix. The Bible Revised standard version. Tsh. 15,000/=
x. Advanced learner’s Dictionary by OXFORD. Tsh. 40,000/=
xi. Kamusi Sanifu ya Kiswahili by TUKI. Tsh. 20,000/=
xii. Atlas. Tsh. 22,000/=
SEHEMU C: ANGALIZO KWA MZAZI/MLEZI
(i) Fedha yoyote itakayolipwa kwa mhasibu haitarudishwa tena kwa mteja
(ii) Shule inafuata mihula inayotolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, hivyo
itakuwa na mihula mirefu miwili na mifupi miwili kwa mwaka. Mzazi/mlezi
unaombwa kutoa ushirikiano wako kuhakikisha mtoto anawasili kwa wakati shuleni,
vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.
(iii) Mawasiliano yoyote kati ya mwanafunzi na mzazi/mlezi yafanyike kwa kupitia Mkuu
wa shule makamu mkuu wa shule, ofisi ya Taaluma na ofisi ya Malezi. Mwanafunzi
haruhusiwi kuwa na simu ya mkononi awapo shuleni.
(iv) Shule haina utaratibu wa mzazi/mlezi kumwona mwanafunzi isipokuwa mzazi ataitwa
na uongozi wa shule kama kuna ulazima wa kufanya hivyo
(v) Mzazi/mlezi unashauriwa kutompa mtoto fedha nyingi ambazo zitamfanya apoteze
utulivu wa maisha ya shule na kuvunja sheria za shule.
(vi) Shule ina utaratibu wa kushughulikia usafiri kwa wanafunzi wanaotoka mbali kipindi
shule inapofunga. Hivyo, mzazi/mlezi utapewa taarifa kabla ya shule kufunga.
(vii) Mzazi hakikisha unapima afya ya mwanao kwa uaminifu na kutoa taarifa za kweli kwa
mwanafunzi mwenye matatizo ya kiafya kwenye uongozi wa shule na kwenye fomu
(Medical Examination Form) ili kuepuka usumbufu wakati wa masomo. Mwanafunzi
mgonjwa atapewa huduma ya kwanza katika zahanati ya shule na endapo atazidiwa
atapelekwa hospitali.
(viii) Shule haitoi chakula maalumu (special diet) kwa mwanafunzi mgonjwa.
(ix) Mzazi/mlezi huruhusiwi kumletea mwanafunzi chakula cha aina yoyote kutoka nje ya
shule.
Nakutakia Baraka za Mungu na maandalizi mema.
_ J.KAMETE
MKUU WA SHULE
Ukurasa wa 6 kati ya 15
SEHEMU D: MAELEZO JUU YA TAARIFA BINAFSI ZAMWANAFUNZI
(IJAZWE NA MZAZI /MLEZI NA KURUDISHWA SHULENI)
1. JINA LA MWANAFUNZI ------------------------------------------------------------------------
2. JINSIA: KE -------------------------------------------------
3. TAREHE YA KUZALIWA ----------------- MWEZI --------------- MWAKA ---------------
WILAYA ----------------------------------------- MKOA --------------------------------
NCHI ------------------------
4. NINI MALENGO YAKO YA KUSOMA? (Unataka kuja kuwa nani katika maisha yako baada
ya masomo?)………………………………………………………………………..
……………………………………………………………………………………………..
5. DINI-----------------------------------
6. KABILA ---------------------------------------------
7. URAIA -----------------------------------------------
8. JINA LA MZAZI/MLEZI -------------------------------
ANUANI ----------------------------------------
SIMU --------------------------------------------
HISTORIA YA MWANAFUNZI
1. JINA LA BABA ----------------------------------------------------
2. JINA LA MAMA -------------------------------------------------
3. JINA KAMILI LA MLEZI (AISHIYE MBEYA)
----------------------------------------------------------------------
4. KAZI YA MZAZI/MLEZI (MKULIMA/MFANYAKAZI/MFANYABIASHARA)
-------------------------------------------------
5. TATIZO LA KIAFYA ALILONALO ---------------------------------------------
6. SHULE ALIKOTOKA ---------------------------------------------
7. NAMBA YA MTIHANI______________________________
SHULE WILAYA DARASA MWAKA
Iwapo mzazi/mlezi hapatikani wafuatao utawala waweza kuwasiliana nao (ambao lazima wawe watu
wazima wanaoweza kutoa msaada na taarifa sahihi za mwanafunzi)
NA JINA UHUSIANO ANAPOISHI SIMU
1
2
3
Mimi mzazi/mlezi wa mwanafunzi mtajwa hapo juu nathibitisha taarifa hii ni sahihi.
Sahihi ya mzazi -------------------------------- Tarehe ----------------------------------------
Ukurasa wa 7 kati ya 15
SEHEMU E: TAMKO RASMI LA KUKUBALI NA FASI YA KUJIUNGA NA
SHULE (IJAZWE NA KURUDISHWA SHULENI)
(a) Mimi ______________________________ambaye ni mzazi/mlezi wa
mwanafunzi________________________________nimezisoma, nimezielewa na
kukubali taratibu na sharia za shule hii.
(b) Nakubali nafasi niliyopewa ya kidato cha__________ mwaka____________ kwa ajili
ya mtoto wangu.
(c) Naahidi kutekeleza yafuatayo:
i. Kulipa malipo yote kama ilivyoainishwa
ii. Kushirikiana na shule katika malezi na kufuatilia maendeleo ya taaluma ya mtoto
ili aweze kufikia kiwango kizuri cha ufaulu na nidhamu.
iii. Kumuelimisha mtoto kufuata na kutekeleza sheria na taratibu za shule kama
zilivyoainishwa katika fomu ya kujiunga.
(d) Nakubali kuwa nitashirikiana na shule katika kumsimamia mtoto wangu kitaaluma ili
aweze kufikia kiwango cha ufaulu wa zaidi ya wastani wa 60. Chini ya ufaulu huo
itabidi tushauriane.
Sahihi ya mzazi/mlezi___________________ Tarehe___________________
Ukurasa wa 8 kati ya 15
SEHEMU F: SHERIA ZA SHULE
1. Mwanafunzi anatakiwa kuwaheshimu walimu wote na wafanyakazi wasio walimu na mtu
yeyote aliyemzidi umri awapo shuleni na mahali pengine popote hiyo ni pamoja na
kuchuchumaa chini anaposalimia mtu yeyote aliyemzidi umri, pia ni wajibu wake
kumpokea mwalimu/mfanyakazi na mtu yeyote aliyemzidi umri anapopita/kuingia popote.
Kushindwa kufanya hivyo ADHABU KALI ITATOLEWA KWA ATAKAYEENDA
KINYUME NA SHERIA HII.
2. Ni lazima mwanafunzi aoneshe nidhamu ya kiwango cha juu katika maongezi na
wanafunzi wenzake, wazazi wake/walezi wake bila kutumia lugha ya
matusi/chafu/mitaani/kejeli/ubishi/dharau/kuzomea/kufyonza. Kushindwa kufanya hivi
kutasababisha mwanafunzi KUSIMAMISHWA MASOMO/KUFUKUZWA SHULE.
3. Mwanafunzi anatakiwa kuishi kwa amani, heshima, utii usikivu na upendo kwa watu wote,
hivyo hapaswi kupiga/ kupigana kushiriki uovu wa aina yoyote ile popote ikiwa ni kwa
kuona/kusikia, kufanya kosa lolote la jinai. Ni wajibu wake kutoficha siri ya uovu wowote
aliouona/kuusikia, kupatikana na kosa lolote katika haya kutasababisha mwanafunzi huyu
KUFUKUZWA SHULE MOJA KWA MOJA BILA MSAMAHA.
4. Mwanafunzi akikamatwa na makosa yafuatayo; wizi, ulevi, uvutaji sigara, uasherati,
kufanya mapenzi, kujihusisha na mazungumzo ya mapenzi, kusagana, kupata mimba/kutoa
mimba, kutoka au kulala nje ya shule, kuingia kwenye vilabu vya pombe/kumbi za starehe,,
kutumia madawa ya kulevya, kuandikia barua ya mapenzi, Kwa kosa lolote katika hayo
mwanafunzi ATASIMAMISHWA MASOMO/ATAFUKUZWA SHULE MOJA KWA
MOJA BILA MSAMAHA.
5. Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa kofia, viatu vyenye kisigino kirefu, visivyo na kamba,
heleni, mikufu, kanga, bangili, pete, sketi fupi za kubana/mipasuo. Marufuku kufuga
nywele, kupaka rangi kucha au nywele, kujichubua, Yeyote atakayepatikana na haya
atarudishwa nyumbani kumleta mzazi au mlezi pamoja na ONYO KALI.
6. Mwanafunzi haruhusiwi kumiliki simu, redio, kamera, CD, DVD, pasi, hita, mshumaa,
silaha yoyote mfano kisu, chupa. Aidha, kuwa na dawa za aina yoyote bwenini, kwa kila
kosa adhabu yake ni KUFUKUZWA SHULE BILA MSAMAHA.
7. Mwanafunzi anatakiwa kuvaa sare wakati wote awapo darasani, atokapo nje ya Shule
aendapo kanisani, aingiapo shuleni, anaposafiri kuja shuleni, aendapo hospitali, kushindwa
kufanya hivyo ni kosa linalosababisha mwanafunzi KUFUKUZWA/KUSIMAMISHWA
SHULE.
8. Shule yetu ni ya Kikristo, hivyo mwanafunzi anatakiwa kufuata taratibu zetu kuhusiana na
ibada na vipindi vya dini. Kushindwa kutii ni kosa ambalo halitavumiliwa na adhabu yake
ni KUFUKUZWA SHULE.
9. Ni marufuku mwanafunzi kuletewa chakula chochote kutoka nje ya Shule kwa sababu za
kiusalama, Pia haruhusiwi kupokea na kuongea na mgeni yeyote, Mzazi au Mlezi
aliyeandikishwa na kutambulishwa na ofisi ndiye anayeweza kuonana na mwanafunzi ikiwa
ulazima utajitokeza ataruhusiwa. Aidha, Mzazi/Mlezi huruhusiwi kuonana na mwanafunzi
na hatuna siku maalumu ya kuja kumuona mwanafunzi (visiting day) kukiuka sheria hii
ADHABU KALI ITACHUKULIWA.
Ukurasa wa 9 kati ya 15
10. Ni lazima mwanafunzi aripoti Shule inapofunguliwa na isizidi saa nane kamili mchana.
Mwanafunzi anayechelewa hatapokelewa badala yake ATARUDISHWA NYUMBANI
KUMLETA MZAZI.
11. Ni wajibu wa mwanafunzi kushiriki kazi za mikono mf. Usafi wa mazingira, kufyeka
(kufagia), Ujenzi kilimo. Kukataa kufanya hivyo ADHABU KALI
ITATOLEWA/KUMLETA MZAZI.
12. Mwanafunzi haruhusiwi kuvaa ndala/viatu vya wazi (open shoes) popote isipokuwa
bwenini tu. Kukiuka hivyo ADHABU KALI ITACHUKULIWA.
13. Mwanafunzi anatakiwa kuheshimu Bendera ya Taifa, Nembo ya Taifa, Wimbo wa Shule,
Fedha na picha za Viongozi na alama nyingine za Taifa. Aidha, kuheshimu miito yote ya
kengele, Kutofanya hivyo ADHABU KALI ITACHUKULIWA.
14. Mwanafunzi anatakiwa kuwa safi wakati wote, kulala katika sehemu aliyopangiwa kwa
wakati unaotakiwa, kutolala wawili kitanda kimoja na kuhakikisha kuwa bweni lake na
darasa ni safi wakati wote ikiwa pamoja na sehemu ya kulia chakula na ukumbi. Kushindwa
kufanya hivyo ni kosa na ADHABU KALI ITATOLEWA.
15. Mwanafunzi haruhusiwi kufanya mawasiliano na Mzazi /Mlezi bila ruhusa ya uongozi wa
Shule, pia mwanafunzi anatakiwa kuomba, kibali maalumu endapo kutakuwa na tatizo
litakalomlazimu mwanafunzi kuhudumiwa nje ya Shule. Kutofanya hivyo kutasababisha
KUSIMAMISHWA SHULE/KUMLETA MZAZI.
16. Mwanafunzi anatakiwa kufanya bidii sana katika masomo/darasani, mwanafunzi mvivu
hatavumiliwa, endapo atashindwa kufikisha kiwango cha alama zilizowekwa na uongozi wa
Shule (wastani wa alama 50 kidato cha kwanza, cha pili, cha tatu kwenda cha nne na kwa
kidato cha tano kwenda cha sita ni lazima mwanafunzi afikishe ufaulu wa daraja la pili
(Division Two) vinginevyo ANAPASWA KUMLETA MZAZI.
17. Mwanafunzi hapaswi kupiga kelele anapokuwa katika mazingira ya Shule (yaani darasani,
bwenini, mesini) na asitoke bila ruhusa ya mwalimu au kiongozi aliyepo, Aidha,
mwanafunzi anatakiwa kuhudhuria Shule muda wote wa masomo ndani na nje ya darasa
(Ruhusa yoyote ya kutohudhuria darasani itatolewa na Mkuu wa Shule tu au mwalimu
atakayekuwa ameteuliwa na Mkuu wa Shule mfano: Makamu mkuu wa shule, Mwandamizi
taaluma, Nidhamu n.k. Kukaidi ni makosa hivyo mwanafunzi anaweza KUSIMAMISHWA
AU KUFUKUZWA SHULE.
18. Mwanafunzi anatakiwakuhudhuria na kuheshimu maandalizi ya jioni na asubuhi (Night and
Morniing preparations) Kushindwa kufanya hivyo mwanafunzi anatakiwa akamlete
Mzazi/Mlezi na ADHABU KALI ITATOLEWA.
19. Mwanafunzi mwenye matatizo ya kiafya atatakiwa aoneshe cheti cha tatizo lake mara
anapo ripoti Shule au apatapo hicho cheti cha daktari wa hospitali ya serikali au hospitali
inayotambuliwa ndicho kitakachokubalika kuoneshwa kwa Nesi wa Shule, matron au
mwalimu mwandamizi nidhamu. Kinyume na hivyo AMLETE MZAZI.
20. Mwanafunzi haruhusiwi kuandika maandishi kitabuni, katika dawati, meza, viti, au kwenye
kuta za majengo ya Shule. Kukaidi kutii hilo ni makosa hivyo mwanafunzi anaweza
KUSIMAMISHWA AU KUFUKUZWA SHULE.
Ukurasa wa 10 kati ya 15
21. Mawasiliano yote ya mwanafunzi awapo shuleni yatakuwa kwa lugha ya KIINGEREZA.
Hivyo ni wajibu wake kujifunza lugha hiyo kwa bidii na kuongea muda wote. Kutozingatia
hili MWANAFUNZI ATAPEWA ONYO KALI/ KUSIMAMISHWA MASOMO.
22. Matatizo au mapendekezo yawasilishwe kwa kupitia serikali ya wanafunzi au uongozi wa
Shule kukiwa na tatizo lolote kwa ufumbuzi wa mara moja, Uongozi hautavumilia
mwanafunzi yeyote atakayejihusisha na maandamano au migomo ya aina yoyote. Kufanya
kosa hilo kutasababisha mwanafunzi KUFUKUZWA SHULE MOJA KWA MOJA BILA
MSAMAHA.
23. Ni lazima mwanafunzi aamke na kulala kwa wakati na muda uliopangwa na uongozi wa
Shule, Vinginevyo mwanafunzi atarudishwa kumuita mzazi/mlezi wake na ADHABU
KALI ITATOLEWA DHIDI YAKE.
24. Ni wajibu wa mwanafunzi kulinda mali zote za Shule kama dawati na meza anayokalia,
vifaa vya usafi, kutokuharibu majengo ya shule na samani zote, vinginevyo itamlazimu
kulipia mali yoyote ya shule atakayoharibu iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya.
Kushindwa kufanya hivyo atapaswa AMLETE MZAZI PAMOJA NA FIDIA.
25. Mwanafunzi haruhusiwi kukata mti katika mazingira ya Shule, na kutunza mazingira hayo
ni wajibu wake, kuokota karatasi pale anapoziona na kutotupa karatasi ovyo. Kushindwa
kufanya hivyo kutamfanya mwanafunzi KUSIMAMISHWA MASOMO/KULIPIA MTI
ALIOUKATA.
26. Mwanafunzi anatakiwa kuhudhuria darasani muda wote wa masomo awapo shuleni hivyo
hatakiwi kuonekana bwenini wakati wa vipindi/masomo pasipo ruhusa kutoka kwa uongozi
wa Shule. Vinginevyo ATARUDISHWA NYUMBANI KUMUITA MZAZI na ADHABU
KALI ITATOLEWA.
27. Mwanafunzi haruhusiwi kudanganya katika mitihani yoyote ile iwe ya ndani au nje,
kufanya kosa hilo kutasababisha mwanafunzi KUFUKUZWA SHULE KABISA BILA
MSAMAHA.
28. Ni marufuku mwanafunzi kutembelea au kuingia nyumbani kwa mwalimu au wafanyakazi
wasio walimu bila ruhusa maalumu. Pia huruhusiwi kuingia jikoni isipokuwa kwa kibali
maalumu. Kukaidi hili HATUA KALI ZA KINIDHAMU ZITACHUKULIWA PAMOJA
NA KUMUITA MZAZI.
29. Ni kosa kwa mwanafunzi kumkimbia mwalimu au mfanyakazi yeyote, aidha kumgomea
mwalimu, Mfanyakazi asiye mwalimu au kiongozi, kosa hili litamsababishia mwanafunzi
KUSIMAMISHWA MASOMO AU KUFUKUZWA SHULE.
30. Mwanafunzi anatakiwa kuzingatia muda uliopangwa, hii ni pamoja na kuwepo eneo husika
kwa muda husika. Vinginevyo ADHABU KALI ITATOLEWA JUU YAKE.
31. Mwanafunzi haruhusiwi kuingia bwenini na chakula au sehemu nyingine yoyote isiyo
rasmi kulia chakula. Kufanya hivyo ADHABU KALI ITATOLEWA.
Ukurasa wa 11 kati ya 15
SEHEMU H: ANGALIZO KWA MWANAFUNZI
1. Mwanafunzi haruusiwi kupokea kitu chochote kutoka kwa mtu yeyote kutoka nje ya shule
pasipo ruhusa ya ofisi husika hii ni pamoja na kufanya mazungumzo na mgeni yeyote.
2. Mwanafunzi anatakiwa kufanya bidii katika masomo na kuhakikisha anafikisha wastani wa
60 katika mitihani yake yote.
3. Mwanafunzi haruhusiwi kuandika maandishi katika samani za shule, (meza, viti, dawati),
kuta za shule na vitabu.
4. Mwanafunzi hatakiwi kupita eneo lisilo la barabara maalumu na kutupa takataka maeneo
yasiyo rasmi au kuziona na kutoziondoa, pia haruhusiwi kukata miti katika mazingira ya
shule.
5. Mwanafunzi hatakiwi kutembea kilegevu katika eneo la ukakamavu.
6. Ni marufuku kwa mwanafunzi kutembelea sehemu zifuatazo isipokuwa kwa kibali maalum.
i) Ofisi ya walimu (staffroom)
ii) Ofisi za shule
iii) Maabara
iv) Jikoni
v) Nyumba za wafanyakazi.
NB: Kukiuka mojawapo ya kanuni na maangalizo haya kutasababisha mwanafunzi
kupewa adhabu kali.
Ukurasa wa 12 kati ya 15
SEHEMU I: FOMU YA UTII WA KANUNI ZA SHULE NA TABIA
NJEMA (IJAZWE NA KURUDISHWA SHULENI)
Mimi____________________________________________(jina kamili) ninatambua wajibu wangu
kama mwanafunzi na ninaahidi
(a) Sita kosa au kuchelewa kipindi chochote darasani bila ruhusa
(b) Kwamba nitatii na kuwaheshimu viongozi wangu wote kuanzia ngazi ya Kiongozi wa
darasa,Viranja wa shule,walimu,watumishi wasio walimu hadi mkuu wa shule
(c) Kwamba nimezisoma na kuzielewa na nitafuata sheria na kanuni zote za shule pamoja na
maelekezo yote yatakayotolewa mara kwa mara na uongozi wa shule.
(d) Kwamba sitatoka nje ya shule bila ruhusa ya uongozi wa shule.
(e) Kwamba kama nitashindwa kufuata hayo yote hapo juu, hatua kali ichukuliwe dhidi yangu
ambayo ni pamoja na kufukuzwa shule au kusimamishwa masomo .
Tarehe…………………… ………………………………………………….
Jina na sahihi ya mwanafunzi
Tarehe……………………. ………………………………………………
Jina na sahihi ya shahidi mzazi/mlezi
Tarehe…………………… ………………………………………………..
Sahihi ya mkuu wa shule
Ukurasa wa 13 kati ya 15
HHHAAARRRRRRIIISSSOOONNN UUUWWWAAATTTAAA GGGIIIRRRLLLSSS’’’ SSSEEECCCOOONNNDDDAAARRRYYY SSSCCCHHHOOOOOOLLL
Email: [email protected]
Website: www.uwata.org
“EDUCATION IS A SUSTAINABLE ASSET”
______________________________________________________________________________
MEDICAL EXAMINATION FORM
This form consists of section A to be completed by the applicant and section B to be completed
by a registered medical doctor from a recognized government hospital. The completed form
must be submitted along with other application materials.
(Please write in block letter ) .PERSONAL INFORMATION
Full name First Middle Last
Date of
birth
……../………/…….. ………LEVEL
II PAST MEDICAL HISTORY
(I)NERVOUS SYSTEM)
Any loss of consciousness ?Yes/No
If yes, date of incident_____________________
Current treatment_________________________
Any fits? Yes/No
If yes ,type of
fits__________________________
Date of last episode______________________
Current treatment_________________________
(II)MUSCULO-SKELETON SYSTEM
Any deformity? Yes/No
If yes ,which part of the body________________
Use of accessory or aids____________________
(III) OTHER CHRONIC CONDITIONS
HIV/AIDS? Yes/No
If yes ,current treatment____________________
Skin disease? Yes/No
If yes ,which type________________________
Current treatment_________________________
Allergies? Yes/No
If yes ,date of last reaction__________________
Cause of reaction_________________________
Asthma? Yes/No
If yes, when detected __________________
Current treatment____________________
Any heart disease? Yes/No
If yes what disease? ___________________
Current treatment_____________________
Major surgeries? Yes/No
If yes type of surgery__________________
Date of surgery _______________________
Any dietary restrictions? Yes/No
If yes, state restriction__________________
Any history of peptic ulcer disease?
Yes/No
If yes, current treatment________________
III.DECLARATION
I declare that all the information provide above is true to the best of my knowledge
Signature…………… Date……/…../………
SECTION A (TO BE COMPLETED BY THE APPLICANT)
Ukurasa wa 14 kati ya 15
SECTION B
(TO BE COMPLETED BY REGISTERED MEDICAL DOCTOR)
A.PHYSICAL EXAMINATION
1. Skin disease__________________________________________________________________
2. Eye conjunctiva Pupils
Sight: Without glasses Right _______________________________
Left _______________________________
With glasses Right ________________________________
Left________________________________
3. Please state condition of ears (if any discharge) ___________________________________
Mouth and throat _____________________________________________________________
4. Respiratory system:
Any abnormality? ______________________________________________________________
5. Cardiovascular system
Blood pressure: systolic___________________________________________________________
Diastolic_________________________________________________________
Heart: any murmur? Yes/No
If yes which type? _______________________________________________________________
6. Abdomen
Masses_________________________________________________________________
Liver _______________________________________________________________
Spleen _______________________________________________________________
Kidneys ______________________________________________________________
Any operation scars_____________________________________________________
7. Any clinical evidence of gastric /duodenal ulcer?________________________________
B. LABORATORY TEST
1. Urine pregnancy test________________________________________________________
2. Urinalysis
Albumin___________________________________________________________
Sugar_____________________________________________________________
Leukocytes _______________________________________________________
Bilharzia___________________________________________________________
3. Stool analysis____________________________________________________________
4. Blood examination: Hemoglobin__________________________________________________
White blood cell count total____________________________________
Different count:
(a) Neutrophils ___________________________________________
(b) Lymphocytes _________________________________________
(c) Monocytes____________________________________________
(d) Basophils ____________________________________________
(e) Eosinophils ___________________________________________
Ukurasa wa 15 kati ya 15
I have examined Miss ______________________________________And consider that she is not/fit
to be admit to school (Delete which is not applicable)
________________________________
_________________________
DATE SIGNATURE
Authorized Medical Practitioner: Name___________________________________________
_________________________ ________________________________
Title Qualification Address________________________________ ________________________
_______________________________
________________________________ Official stamp or seal
_______________________________
SECTION C :CONCLUSION